22 Aprili 2025 - 21:06
Maandalizi na uhamasishaji wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 2025 / 1446H - Hawzat Imam Ali (as) Tanga - Tanzania

Hawzat Imam Ali (a.s) iliyopo chini ya Taasisi ya Bilal Muslim Mission Tanga, Tanzania, Kitengo cha uhamasishaji wa Michango ya uwezeshaji wa masira ya Imam Husein (a.s), Leo hii Jumatatu 21/04/2025, kimekutana na Waumini wa Bilal Muslim Bushiri na kuongea nao kuhusiana na Suala la Masira ya Imam Hussein (as) mwaka huu wa 1446H. Lengo la ziara hii, ni kuhamasishana zaidi na kuelezea umuhimu wa kutoa Sadaka hasa katika kuichangia Masira ya Imam Husen (a.s).

Katika ziara hii, Samahat Sheikh Swaleh AbduRahmani amewaeleza Waumini juu ya fadhila za kutoa Sadaka na ubora wake.

Tanbihi:

Kitengo hiki cha uhamasishaji kitaendelea na ziara hizi mpaka ndani ya Mwezi wa Muharram Insha'Allah.

Waliofanikisha Ziara hii:


1_Samahat Sheikh Swalehe.
2_Samahat Sheikh Murshid Tibaijuka.
Ripoti hii imetolewa kwa hisani kubwa ya:

Kitengo cha Ripoti  za Tabligh Hawzat Imam Ali (a.s).

Your Comment

You are replying to: .
captcha